Taasisi ya Kuratibu, Kustawisha na Kuhimiza Shughuli za Qurani Iran inayofungamana na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu imetoa taarifa na kulaani hatua ya kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Taarifa hiyo imesema:
"Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga." (Qurani Tukufu 3:54)
Kitendo kichafu na cha kishenzi cha kuivunjia heshima Qurani Tukufu kilichotekelezwa na kasisi mamluki wa kanisa moja huko Florida Marekani ni njama iliyotekelezwa kwa mpango maalumu na vituo vyenye chuki dhidi ya Uislamu. Hakuna shaka kuwa nyuma ya vitendo kama hivyo cichafu ni madola ya kibeberua na taasisi za Kizayuni kwa lengo la kuhujumu Uislamu na Waislamu.
Ni wazi kuwa mataifa ya Waislamu duniani hayatanyamazia kimya hatu ahiyo ya kuvunjiwa heshima kitabu chao kitukufu. Serikali ya Marekani na wale waliotekeleza kitendo hicho cha kishenzi watajuta vitendo vyao.
Taasisi ya Kuratibu, Kustawisha na Kuhimiza Shughuli za Qurani Iran inalaani kitendo hiki cha kuvunjia heshima dini na inatoa wito kwa kufikishwa kizimbani waliotekeleza kitendo hicho.
766236