IQNA

Dharau dhidi ya Qur'ani, alama ya misimamo ya kupindukia mipaka katika baadhi ya jamii

11:13 - March 29, 2011
Habari ID: 2098785
Sayyid Yusuf Ridha Gilani, Waziri Mkuu wa Pakistan amesema kuwa dharau iliyofanyiwa Qur'ani Tukufu kwa kuchomwa moto katika kanisa moja huko katika jimbo la Florida nchini Marekani inabainisha wazi mielekeo ya kuvuka mipaka katika baadhi ya jamii.
Katika taarifa rasmi aliyotoa hapo jana Jumatatu, Sayyid Yusuf Gilani amelaani vikali kitendo hicho cha Kasisi Terry Jones cha kukosea heshima Qur'ani Tukufu. Amesema kitendo hicho cha aibu na kuchukiza kinabainisha wazi misimamo ya kupindukia mipaka ya baadhi ya jamii za Magharibi dhidi ya mafundisho ya Kiislamu. 766931
captcha