Akibainisha jambo hilo, Ali ad-Dabagh, Msemaji wa Serikali ya Iraq amesema kuwa tayari mipango ya kukaribisha na kumlaki Waziri Mkuu Erdogan katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Najaf imekwishakamilika. Maafisa wa ngazi za juu wa serikali, kimkoa na wa Haram Tukufu ya Imam Ali watashiriki katika hafla ya kumlaki kiongozi huyo wa Uturuki. Waziri Mkuu Erdogan aliwasili nchini Iraq hapo jana Jumatatu kwa madhumuni ya kuonana na kuzungumza na viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo kuhusu masuala mbali mbali ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja za uchumi, siasa, biashara na utamaduni. Alipowasili alilakiwa na Nuri al-Maliki, Waziri Mkuu wa Iraq. 766916