Kwa mujibu wa gazeti la Jordan Post, kikao hicho kilianza Aprili Pili kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kuhuisha Hadithi na Turathi Jordan.
Wasomi 22 kutoka Jordan, Saudi Arabia, Sudan, Iraq na Kuwait wanashiriki katika kikao hicho ambacho kinajadili umuhimu wa Seerah ya Mtume SAW katika kukuza shakhsia ya Muislamu.
Fathi Malkawi, mmoja wa waandalizi amesema washiriki watajadili pia namna marejeo ya Seerah yanaweza kutumiwa katika malezi ya Muislamu.
Kikao hicho kimemaliza kazi zake Aprili tatu.
767960