IQNA

Karzai: waliochoma moto Qur’ani nchini Marekani washtakiwe

14:05 - April 04, 2011
Habari ID: 2100398
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan ameitaka Marekani na Umoja wa Mataifa kuwapandisha kizimbani wale wote waliohusika na uchomaji moto wa nuskha kadhaa za Qurani Tukufu nchini Marekani.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa la Afghanistan, kikao ambacho kilihudhuriwa pia na Kamanda wa vikosi vya Nato na Balozi wa Marekani mjini Kabul, Rais Karzai amemtaka Rais na Baraza la Kongresi la Marekani kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Kasisi wa Kimarekani aliyehusika na uchomaji moto wa Qurani Tukufu. Aidha ameitaka serikali ya Marekani kuzuia vitendo vinavyoyavunjia heshima matukufu ya Waislamu duniani. Rais Karzai amesema kuwa, maandamano ya wananchi wa Afghanistan ya kulaani uchomwaji moto Qurani Tukufu ni haki ya kimsingi ya wananchi na akavitaka vikosi vya usalama nchini humo kuweka ulinzi maalumu kwa shabaha ya kudhaminiwa usalama wa waandamanaji.

768384
captcha