Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa la Afghanistan, kikao ambacho kilihudhuriwa pia na Kamanda wa vikosi vya Nato na Balozi wa Marekani mjini Kabul, Rais Karzai amemtaka Rais na Baraza la Kongresi la Marekani kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Kasisi wa Kimarekani aliyehusika na uchomaji moto wa Qurani Tukufu. Aidha ameitaka serikali ya Marekani kuzuia vitendo vinavyoyavunjia heshima matukufu ya Waislamu duniani. Rais Karzai amesema kuwa, maandamano ya wananchi wa Afghanistan ya kulaani uchomwaji moto Qurani Tukufu ni haki ya kimsingi ya wananchi na akavitaka vikosi vya usalama nchini humo kuweka ulinzi maalumu kwa shabaha ya kudhaminiwa usalama wa waandamanaji.
768384