Rais huyo wa Ujeruani amelaani kitendo hicho alipokuwa akikagua kituo kimoja cha kijeshi kilichoko mashariki mwa nchi hiyo. Wulff amewataka watu wote duniani kuheshimiana na kuishi pamoja kwa amani. Kabla ya hapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani pia alilaani uchomaji moto wa Qur'ani uliofanywa na kasisi huyo mwovu nchini Marekani na kuongeza kuwa serikali ya Berlin inapinga vikali harakati kama hizo za kichochezi na dharau dhidi ya matukufu ya kidini. Viongozi wawili hao wa Ujerumani wamechukua msimamo wa kulaani kitendo hicho katika hali ambayo Kansela Angela Merkel mwenyewe ameamua kukaa kimpya na kutozungumzia kabisa jambo hilo. Baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo wamemtuhumu kiongozi huyo kuwa anapuuza masuala yanayowahusu Waislamu. 769265