IQNA

Wabunge Iran walaani ukandamizaji wa Waislamu Mashariki ya Kati

10:36 - April 07, 2011
Habari ID: 2101938
Bunge la Iran yaani Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu imelaani jinai zinazotekelezwa na watawala wa baadhi ya nchi za eneo dhidi ya wananchi.
Katika taarifa yao Wabunge zaidi ya 200 wamesema leo ulimwengu wa Kiislamu unaomboleza mauaji ya kinyama dhidi ya raia huko Libya, Yemen na Bahrain.
Wamesema kuwa nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binaadamu zimepuuca na kunyamazia kimya mauaji ya kinyama katika eneo na kuongeza kuwa jinai hizo zinafanyika kwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani na Uingereza.
Wabunge wa Iran wameitaka Saudi Arabia kuondoa vikosi vyake vamizi nchini Bahrain.
769984
captcha