Baraza la utendaji la Makanisa ya Baptist Marekani limesema kitendo cha kuchoma moto Kitabu Kitakatifu cha Waislamu kilichofanywa mnamo Machi 20 chini ya usimamizi wa Terry Jones wa kanisa la Dove World Outreach Centre katika eneo la Gainesville, Florida ni jambo linalokiuka amri ya Yesu (Nabii Issa AS) ya ‘kumpenda jirani yako kama tunavyojipenda’.
Taarifa hiyo imesema, “Kitendo cha hivi karibuni cha kuchoma moto Qurani katika kanisa moja hakiwakilishi jamii kubwa ya Wakristo Marekani. Ni kitendo tunachokichukua na kimepeleteka tusisitize tena msimamo wa kihistoria wa kanisa la Baptist wa kufungamana na uhuru wa watu wote na dini zote”.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni mhubiri mwenye misimamo mikali wa Marekani Wayne Sapp aliteketeza Qurani Tukufu katika kanisa moja mjini Florida. Kasisi Terry Jones mwenye chuki kubwa dhidi ya Uislamu aliyepanga kuichoma moto Qurani mwaka jana alihudhuria kikao hicho cha jinai.
Waislamu na wasiokuwa Waislamu kote duniani wanaendelea kulaani kitendo hicho cha jinai.
771175