Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran, kikao hicho kimeandaliwa kwa ushirikiano na Idara ya Maulamaa wa Kiislamu wa jamhuri hiyo.
Hii ni duru ya nne ya kikao hicho cha kimataifa ambacho kitafanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Chechnya Ahmad Haji Kadyrov.
Katika mkutano na Maulamaa wa Kiislamu wa maeneo mbali mbali ya Chechnya, Mufti wa Jamhuri ya Tatarstan amesisitiza umuhimu wa kikao hicho kufanyika kwa kiwango cha juu. Pembizoni mwa kikao hicho kutafanyika mashindano ya qiraa ya Qurani Tukufu.
Jamhuri ya Chechnya ni sehemu ya Shirikisho la Russia na iko katika eneo la Caucasus Kaskazini katika eneo la kusini mashariki mwa Bara Ulaya.
Zaidi ya asilimia 95 ya wakaazi milioni moja laki moja wa Chechnya ni Waislamu
770793