Hafla hiyo ijulikanayo kama Al Hijab imeandaliwa na jumuiya hiyo kwa mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwake mwaka 2004 kutokana na kuongezeka wanawake wanaovaa Hijabu.
Wasichana walio kati ya umri wa miaka 7-16 na familia zao kutoka maeneo 10 ya lageria walishiriki katika hafla hiyo ambapo walipewa zawadi za Misahafu na mavazi ya Kiislamu.
Mji wa Constantine ni wa tatu kwa ukubwa na uko kaskazini mashariki mwa Algeria na ni maarufu kama 'Mji wa Tai'. Baadhi ya wanahistoria wanaamini kubwa harakati ya mabadiliko Algeria katika karne ya 20 ilianzia mjini humo kupitia Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu chini ya uongozi wa Al Sheikh Abdul Hamid bin Badis.
772182