Sion Owens mwanachama mwandamizi wa chama cha BNP na mgombea kiti katika uchaguzi wa bunge la eneo la Welsh ametiwa nguvuni akichoma moto Qurani Tukufu katika bustani lake.
Hivi sasa wanasiasa wenye misimamo mikali Ulaya na Marekani wanachezea hisia za wafuasi wao kwa kueneza chuku dhidi ya Waislamu na Uislamu katika jamii ambazo zinawachukia wageni.
Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia nchini Uingereza anapanda wimbi la chuki dhidi ya Uislamu miongoni mwa watu wasio na elumu nchini Uingereza wasio fahamu mafundisho ya Kiislamu.
Kumekuwepo na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Maghairbi ambazo zimechochewa na wanasiasa wanaotafuta kisingizio cha kufeli sera zao za kiuchimi na kijamii.
772419