IQNA

Kozi ya Qurani kwa Waislamu Mashia nchini Zambia

15:10 - April 11, 2011
Habari ID: 2104154
Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Zambia kimepanga kozi za kielimu kuhusu Qurani Tukufu maalumu kwa Waislamu Mashia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Zambia, kozi hizo zitafanyika kwa ajili ya watoto na vile vile watu wazima wenye uwezo duni wa kifedha katika miji mbali mbali nchini humo ikiwemo Katuba.
Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran litatoa suhula zinazohitajika katika kozi hizo ikiwa ni pamoja na waalimu.
Washiriki watafundishwa hifdhi na qiraa ya Qurani Tukufu. Mafundisho hayo yanafanyika kwa lengo la kueneza utamaduni wa Qurani Tukufu katika maeneo husika.
771694
captcha