Sherehe hizo zimehudhuriwa na wageni kadhaa akiwemo Balozi wa Iran nchini Zimbabwe na afisa mwandamizi wa Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu nchini Iran Bw. Masudpur.
Akihutubi katika hafla hiyo Bw. Masudpur ameashiria sifa za kipekee za Bibi Zainab SA kama vile subira kwa mtazamo wa Kiislamu. Amemtaja Bibi Zainab SA kuwa kigezo bora kwa wote.
Naye Mkuu wa Jumuiya ya Walebanon Nchini Zimbabwe Abu Khalil Badir ametoa hotuba iliyoangazia nafasi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kuleta mwamko wa Kiislamu dunani. Amesema Waislamu duniani na hasa Mashia nchini Lebanon wamepata ilhamu kutoka Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo chimbuko lake ni mafundisho ya Kiislamu na Ahlul Bayt AS.
771727