Mashindano hayo yaliyopangwa kuendelea kwa siku nne yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiislamu ya Senegal. Akibainisha malengo ya mashindano hayo, Abdallah Basifr, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Hifdhi ya Qur'ani amesema kwamba malengo hayo ni pamoja na kuvutia uzingatiaji wa Qur'ani na kuwashawishi vijana wa Kiafrika wahifadhi, kusoma na kutadabari kitabu hicho kitakatifu. 771537