Mwambata wa Utamaduni wa Iran Lebanon Mohammad Hussein Raiszadeh amesema umoja wa Kiislamu haumaanishi mtu kuacha madhehebu yake bali ni kuhakikisha maslahi ya pamoja yanazingatiwa huku Waislamu wakiwa na misimamo ya pamoja.
Ameyasema hayo mjini Beirut, alipokutana na mjumbe wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu. Afisa huyo wa Iran amewahimiza Waislamu kusimama pamoja dhidi ya adui wao wa pamoja ambaye ni Utawala wa Kizayuni.
Akizungumza katika mkutano huo Bi. Efaf Hakim ambaye anasimamia kitengo cha wanawaka katika harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sera zake za kuhimiza umoja na mshikamano wa Kiislamu duniani kama vile kutetea haki za Wapalestina, Kuadhimisha Wiki ya Umoja , Siku ya Quds n.k.
772219