IQNA

Kongamano la Watumishi wa Qurani kufanyika Iran

10:29 - April 13, 2011
Habari ID: 2104893
Kongamano la Pili la Watumishi wa Qurani litafanyika Aprili 14 katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran mkoani Khorassan Razavi.
Hujjatul Islam Hassan Azizi, Katibu Mkuu wa Kamati ya Kutafsiri Qurani ya Chuo cha Mkoa wa Khorassan Razavi amesema kongamano hilo litafanyika kwa lengo la kuwaenzi wanaume na wanawake wanaohudumia Qurani Tukufu.
Amesema wanazuoni na wasomi wa Chuo cha Kidini cha Qum akiwemo Hujjatul Islam Mahmoud Rajabu watahutubia kongamano hilo.
Amesema vigezo vilivyotumiwa kuwaenzi watumishi bora wa Qurani ni pamoja na utafiti kuhus tafsiri na sayansi za Qurani, usimamizi bora (menejmenti) kwa mujibu wa Qurani Tukufu na vile vile ubunifu uliotegemea misingi ya Qurani.
Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.
772342

captcha