Mohammad Ali Asadtash Mkurugenzi wa Masuala ya Qurani katika Chuo Kikuu cha Qum amesema kuwa warsha hiyo itakuwa ikifanyika kila wiki siku za Jumanne na Jumatano jioni.
‘Warsha hii itaendelea kwa wiki tano na itajumuisha vikao 10 vitakavyoongozwa na mwanafunzi wa shahada ya Uzamili anayesoma lugha ya Kiingereza hapa chuoni’.
Ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Qum kinapanga kuandaa duru ya 29 ya mafunzo ya Qurani Tukufu maalumu kwa waalimu wa Qurani. Aidha kozi za kutafakari Qurani Tukufu zitafanyika chuoni hapo kwa ushirikiano wa Taasisi ya Tadabbor.
Vile vile amesema wanachuo bora katika mashindano ya Qurani chuoni hapo watashiriki katika mashindano ya Qurani mjini Isfahan kati mwa Iran yatakayofanyika Aprili 26 na 27.
772978