IQNA

Kikao cha ‘Vijana na Ulimwengu wa Kiislamu’ kufanyika Tehran

10:26 - April 13, 2011
Habari ID: 2104896
Kikao cha kielimu cha ‘Vijana na Ulimwengu wa Kiislamu’ kimepangwa kufanyika hapa Tehran chini ya usimamizi wa Idara ya Utamaduni ya Chuo Kikuu cha Madhehebu ya Kiislamu.
Kikao hicho cha mwezi Septemba kimeandaliwa na wanachuo wa chuo hicho kwa kuzingatia misingi ya ukuruba na umoja wa Kiislamu.
Kati ya maudhui zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni misingi ya umoja na ukuruba wa Kiislamu katika Qurani na Sunnah, usimamizi bora ya ukuruba na umoja katika ulimwengu wa Kiislamu, ukuruba na umoja wa Kiislamu kama hitajio la kijamii na kidini, umoja wa Mashia na Masunni, matatizo na changamoto katika kuleta umoja na ukuruba wa Kiislamu, suluhisho la Qurani katika suala la umoja, mwamko wa Kiislamu, watawala madikteta kama kizingiti cha umoja wa Kiislamu na uchunguzi kuhusu waanzilishi wa umoja wa Kiislamu.
Kikao hicho pia kitakuwa na maonyesho ya vitabu na kazi za sanaa kuhusu umoja wa Kiislamu, mashairi, kaligrafia ya aya za Qurani, hadithi na semi za wanazuoni.
Wanakusudia kushiriki wanapaswa kuwasilisha makala zao kabla ya Juni 10. Walio nje ya Iran wanaombwa kuwasiliana na ubalozi wa Iran ulio karibu nao popote pale duniani.
773031
captcha