Semina hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kuwait kwa ushirikiano wa Kituo cha Qur'ani cha al-Huda kinachofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait. Katika semina hiyo iliyofanyika jana Jumanne Sheikh Fahd al-Kindi alizungumzia fadhila za Qura'ni na udharura wa kutekelezwa mafundisho yake pamoja na umuhimu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na neema zake zisizo na mwisho, na hasa neema ya watu kujaaliwa kuwa Waislamu. Amesema iwapo wanadamu watazingatia vyema mafundisho ya Qur'ani Tukufu, kitabu hicho cha mbinguni kinaweza kuwaongoza kwenye njia nyoofu na kuwaondoa kwenye giza la dhulma na maovu. Amesisitiza umuhimu wa watoto kupewa malezi kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu na kuhimizwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu. 773668