Sheikh Juma Ngao Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Ushauri la Waislamu amesema kuwazuia wasichana Waislamu kuvaa hijabu ni jambo ambalo linakiuka haki za Waislamu.
‘Mafundisho ya Kiislamu yanawataka wanawake na wasichana kujifunika nyuso zao wakiwa shuleni au kazini. Hatahivyo katika shule zinazomilikwa na makanisa, Waislamu wananyimwa ruhusa ya kuvaa hijabu. Tunahisi huu ni ubaguzi dhidi ya watoto Waislamu.
Sheikh Ngano amesema Waislamu wanamiliki shule zao lakini wanapelekea watoto wao pia katika shule zinazomilikiwa na kanisa kwa sababu waalimu katika shule hizo wanalipwa na serikali. Amesema kwa kuzingatia hilo, kutokana na kuwa Waisamu wanalipa kodi basi ni haki ya watoto wao pia kusoma katika shule za Wakristo.
Mwezi Julai mwaka 2009 Wizara ya Elimu ya Kenya ilitoa taarifa na kusema wasichana Waislamu wana haki ya kuvaa hijabu wakiwa shuleni. Wizara hiyo ilisema haki ya kuabudu inazingatiwa katika katiba ya Kenya. Hatahivyo baadhi ya shule zinazomilikiwa na kanisa mjini Nairobi na mji wenye Waislamu wengi wa Mombasa zinaendelea kuwafukuza wasichana Waislamu wanaovaa hijabu.
773764