Ameongeza kuwa kitendo cha kuchoma moto Qurani kinatekelezwa na watu ambao binafsi ni mashetani au shetani amejidhihirisha katika nafsi zao.
Mehmanparast amesema siasa kuu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na matukio na mabadiliko yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuzingatiwa matakwa ya wananchi
Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi Mehamanparast amesema kulazimisha irada na matakwa ya wachache juu ya matakwa ya waliowengi ni udikteta na kuongeza kuwa Iran katu haikubaliani na hatua za ukandamizaji na utumiaji nguvu dhidi ya raia wanaopigania matakwa yao kwa njia ya amani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria himaya na uungaji mkono wa Umoja wa Ulaya kwa kikundi cha kigaidi cha Munafikina maarufu kama MKO katika matukio yaliyojiri kwenye kambi ya kikundi hicho huko nchini Iraq na kuisitiza kwamba kinachotarajiwa kwa mashirika, jumuiya za kimataifa na nchi zinazajinasibu kuwa watetezi wa haki za binadamu ni kuachana na mienendo ya kindumakuwili na ya kisiasa kwa kulaani vitendo vya kigaidi na kuacha kutoa hifadhi kwa magaidi.
Kuhusu hatua ya Saudi Arabia ya kupeleka vikosi vyake huko Bahrain, Mehmanaparast amesema ufumbuzi wa mgogoro katika nchi yoyote ile unapatikana kwa kuandaa mazingira yatakayosaidia katika kuchunguza, kuyatambua na kuyakidhi matakawa ya wananchi; lakini kama njia itakayotumiwa haitokuwa sahihi sio tu matakwa hayo hayatokidhiwa bali mgogoro uliopo utakuwa tata zaidi.
Sambamba na kutahadharisha kuwa endapo serikali zitaitapakaza mikono yao damu za wananchi, zitasababisha majeraha makubwa na makovu yatakayosalia kwa muda mrefu ambayo kuyaondoa kwake kunaweza kusababisha madhara mengi, Mehmanparast ameeleza kuwa sio sawa kwa nchi nyingine kuingilia suala ambalo ni la ndani ya nchi na ambalo linaweza kutatuliwa kwa njia za amani na wananchi wenyewe wa Bahrain.
Kwa upande wa matukio ya Libya, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hali ya Libya ni tata, kwani kwa upande mmoja serikali inawakandamiza wananchi na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi hao wasio na hatia, na kwa upande mwingine kuna nchi za Magharibi ambazo kwa kutumia kisingizio cha kuwasaidia wananchi wa Libya zimejiingiza nchini humo kwa lengo la kulinda manufaa na maslahi yao.
Ama kuhusu matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Saud al Faisal ambaye ameituhumu Iran kuwa inaingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo, Mehamanparast amesema kufuata njia isiyo sahihi na kujitumbukiza kwenye fitna ndiko kunakopelekea kutoa matamshi kama hayo yasiyo na busara wala nadhari. Sambamba na kusisitiza juu ya nukta kwamba ni nchi zenyewe za Mashariki ya Kati tu ndizo zinazoweza kusaidia kupatikana amani na uthabiti katika eneo hili Mehamanparast amesema serikali zote zinapaswa kuhakikisha zinakuwa pamoja na wananchi wao kwani kama zitaamua kufuata njia isiyo sahihi wananchi watajiweka mbali zaidi na serikali hizo, na matokeo yake serikali zitakuwa dhaifu; na ikiwa serikali zitakuwa dhaifu zitaweza kudhuriwa na pigo lolote lile litakalotolewa na utawala wa kizayuni wa Israel.
773064