IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa alaani jinai za Saudia nchini Bahrain

12:26 - April 16, 2011
Habari ID: 2106296
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amelaani mauaji ya raia wasio na hatia huko Bahrain yanayotekelezwa na vikosi vya ufalme wa Saudi Arabia.
Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Ahmad Jannati amesema watawala wa Saudi Arabia hawajawahi kuufyatulia hata risasi moja utawala wa Kizayuni unaowadhulumu Wapalestina lakini wametuma vikosi vya kijeshi Bahrain kuwaua Waislamu nchini humo.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameashiria ushari wa utawala wa kifalme wa Manama katika kuwaua na kuwatesa watu wa Bahrain kwa sababu tu ni Waislamu wa Madhehebu ya Shia. Ameongeza kuwa kumeshuhudiwa mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu zenye watawala madhalimu na kwamba hilo ni jambo ambalo maadui wamekuwa wakihofia kwa miaka mingi.
Ayatullah Jannati ameongeza kuwa maadui wanalenga kuvuruga umoja wa Waislamu kwa kuibua hitilafu za kikabila, kirangi na kisiasa. Ametoa wito kwa mataifa yote ya Kiislamu kuwa angalifu na kuhifadhi umoja chini ya bendera ya Ummah mmoja.
Khatibu wa sala ya Ijumaa akiendelea na hotuba yake amemshukuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kuhusu mauaji ya wananchi wa Bahrain.
Ayatullah Jannati pia ameashiria kutajwa mwaka huu wa Kiirani kuwa mwaka wa Jihadi ya Kiuchumi na kusema unapaswa kuwepo ushirikiano kati ya taasisi za serikali na vyombo vya habari ili kuwezesha mkondo wa ustawi wa kiuchumi kuwa harakati ya pande zote.
774446
captcha