Kwa mujibu wa gazeti Al Watan Online chapa ya Saudia, sherehe za kufunga mashindano hayo zimefanyika Alhamisi Aprili 14 katika sherehe zilizohudhuriwa na Rais Abdullahi Wade wa Senegal na Abdullah Abdulmohsen al-Turki Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu Duniani.
Akizungumza katika hafla hiyo al Turki amesema kwa kuwahimiza watoto Waislamu wahifadhi Qurani, kizazi kipya cha vijana wanazingatia mafundisho ya Kiislamu kitaibuka.
Kwa upande wake rais Wade wametaka mashindano hayo yawe yakifanyika barani Afrika kila mwaka. Amesema mashindano hay ni jawabu kwa wale wanaojaribu kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Mashindano ya kimataifa ya hifdhi na usomaji Qura'ni nchini Senegal yalihudhuriwa na nchi 28. Mashindano hayo yaliyoanza siku ya Jumatatu yaliwashirikisha vijana 3,300 wa umri wa kati ya miaka 12 hadi 20.
Muhammad Sayyid Ba, Katibu Mkuu wa Shirika la Ustawi na Mafunzo ya Kiislamu la Senegal amesema kwamba Senegal imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kutokana na nafasi yake nzuri katika mafunzo ya Qur'ani.
774756