IQNA

Iran yalaani vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya dhidi ya maafisa wake

13:28 - April 17, 2011
Habari ID: 2107079
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani uamuzi wa Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo maafisa kadhaa wa Iran na kusema hatua hiyo ni ya kisiasa ambayo inaonyesha kuwa Umoja wa Ulaya unafuata maagizo ya Marekani.
Jumatano Umoja wa Ulaya ulitangaza vikwazo vipya vya kifedha na marufuku ya kusafiri dhidi ya maafisa 32 wa Iran kwa madai ya kukiuka haki za binaadamu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast amesema vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya ni njama ya kupotosha fikra za walimwengu kuhusu jinai za nchi za Magharibi katika nchi zao na katika eneo hasa Iraq na Afghanistan na vile vile jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina. Aidha alitoa wito kwa nchi za Magharibi kusitisha sera za kindumakuwili na vile vile ziache kuunga mkono ukandamizwaji wa waandamanaji katika baadhi ya nchi. Nchi za Magharibi zimebakia kimya kuhusu jinai zinazotekelezwa na utawala wa Kifalme wa Bahrain dhidi ya raia wanaoandamana kwa amani nchini humo.
775382
captcha