IQNA

Tamasha la kutetea Qur'ani Tukufu lafanyika Baghdad

17:01 - April 17, 2011
Habari ID: 2107224
Tamasha la Qur'ani Tukufu limefanyika mjini Baghdad Iraq kwa madhumuni ya kutetea Qur'ani Tukufu mbele ya dharau iliyofanywa hivi karibuni na Kasisi Teryy Jones wa jimbo la Florida nchini Marekani.
Tamasha hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Shahid Sadr kwa ushirikiano wa Kamati ya Uungaji Mkono kwa Qur'ani Tukufu ya Iraq, lilifanyika katika mtaa wa Sadr mjini humo. Tamasha hilo lililoandaliwa hapo siku ya Ijumaa lilihudhuriwa na wanazuoni, wanafikra wa Kislamu, wasomaji Qur'ani na wanasiasa wa nchi hiyo. Wabunge waliohudhuria tamasha hilo wamesema kuwa bunge la Iraq limeutaja mwaka huu kuwa mwaka wa Qur'ani Tukufu ikiwa ni katika kutetea kitabu hicho kitakatifu na kulaani kitendo cha kasisis Terry Jones cha kukosea heshima kitabu hicho. 775164
captcha