Ayatullah Sistani amelaani vikali jinai zinazofanywa na askari wa Saudia dhidi ya taifa la Bahrain na kusema kuwa jambo hilo linakwenda kinyume na maslahi ya watu wa nchi hiyo. Akizungumzia jambo hilo hivi karibuni, Sayyid Jawad Shahrestani, mwakailishi wa marja huyo katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kiongozi huyo wa kidini amehuzunishwa sana na matukio ya Bahrain na kwamba anafanya juhudi kubwa za kupunguza machungu ya wananchi wa nchi hiyo wanaoendelea kukandamizwa na kuuawa ovyo na askari wa Saudi Arabia wakishirikiana na wa utawala wa Manama. Amesema Ayatullah Sistani anatambua vyema ushirikiano na uhusiano mkubwa uliopo baina ya koo mbili dhalimu za Saudi na Aal Khali. 775156