Ikmal Deen Ihasanoghlou Katibu Mkuu wa OIC atashiriki katika kikao cha Kamati ya Kupambana na Ugaidi ambayo inafungamana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambacho kimepangwa kufanyika kuanzia hapo kesho Jumanne. Katibu Mkuu huyo atazungumza katika kikao cha ufunguzi cha kamati hiyo kitakachoendelea kwa siku tatu ambapo mashirika mengi ya kieneo na kimataifa yatashiriki. Atabainisha nafasi ya kieneo na kimataifa ya OIC katika kupambana na tatizo la ugaidi duniani. 775902