IQNA

Duru ya 16 ya mashindano ya Qur'ani kufanyika Uingereza

12:01 - April 19, 2011
Habari ID: 2108303
Duru ya 16 ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanaume imepangwa kufanyika tarehe 4 Septemba.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya al-Birr yatafanyika katika hatua tatu za hifdhi ya Qur'ani nzima kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 22, hifdhi ya juzuu 20 za kwanza za Qur'ani kwa wale walio na umri wa chini ya miaka 18 na hifdhi ya juzuu 10 za mwanzo za Qur'ani kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 14. Washindi wa kila hatua watatunukiwa zawadi na wasimamizi wa mashindano hayo. Lengo la kufanyika mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuwashawishi vijana wa Kiislamu wanaoishi Uingereza kuhifadhi Qur'ani Tukufu na vilevile kuwaandalia fursa ya kutafakari na kufahamu vyema aya za kitabu hicho kitakatifu. Taasisi ya Qur'ani ya al-Birr ni shirika la masuala ya kheri ambalo huwaandalia watu walio na hamu ya kufahamu mafundisho ya Qur'ni Tukufu fursa ya kufikia lengo hilo kwa urahisi. Taasisi hiyo huandaa mashindano kama hayo kila mwaka. 776176
captcha