IQNA

Kikao cha 'Mfungamano na Watu wa Bahrain' chafanyika Sweden

11:13 - April 20, 2011
Habari ID: 2108946
Kikao cha kutangaza mfungamano na watu wa Bahrain na kulaaniwa hatua za ukandamizaji za askari jeshi wa ufalme wa Aal Khalifa na Aal Soud dhidi yao kilifanyika siku ya Jumatatu huko katika mji wa Stockholm nchini Sweden.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wawakilishi wa Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International, Hilali Nyekundu na mabalozi wa Iraq na Iran pamoja na shakhsia wa kisiasa wa Bahrain na wawakilishi wa vyama vya kisiasa na kisheria wa Baharain. Kikao hicho kimefanyika kwa madhumuni ya kulaani jinai zinazotekelezwa na falme za Bahrain na Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Bahrain wanaopigania haki zao kwa njia ya amani. Washiriki wa kikao hicho wametaka walimwengu kubainishiwa vyema kiwango cha jinai hizo kupitia vyombo vya habari na taasisi husika za kutetea haki za binadamu. Maandamano makubwa yamepangwa kufanyika mbele ya ubalozi wa Suadia nchini Sweden hapo siku ya Jumatatu ijayo kulaani jinai zinazofanywa na askari wa nchi hiyo dhidi ya watu wasio na hatia huko Bahrain. 776973
captcha