Wanachuo wa Kusini mwa Lebanon wamejitokeza kwa wingi kulaani kitendo hicho kilichotekelezwa na Wakristo wenye misimamo mikali.
Maandamano hayo yamefanyika katika hafla ya kuanza kuandikwa Qurani kubwa zaidi duniani katika Chuo Kikuu cha Kimatiafa cha Lebanon. Mwanazuoni wa Kishia wa Lebanon Sheikh Hassan al Zayyat anaandika aya hizo za Qurani zenye urefu wa sentimeta 140 na upana wa sentimeta 72.
Wanafunzi hao wamesema njia bora zaidi ya kulaani kitendo cha kuivunjia heshima Qurani ni kujihusisha zaidi na shughuli za Qurani kama maradi huo wa kuandika Qurani kubwa zaidi duniani.
777794