Kikao hicho cha siku tatu kilichoanza Aprili 20 kinawajumuisha wataalamu 50 wa Qurani kutoka kote Iran na mada kuu itakuwa Qurani kwa mtazamo wa kiutamaduni.
Mkutano huo unaongozwa na Hujjatul Islam Hamid Mohammadi mshauri wa Masuala ya Qurani wa Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu.
Masuala yatakayojadiliwa chini ya mada kuu ni kama vile njia za kutumia Qurani katika ujuzi unaohitajika katika maisha ya kila siku na mbinu mpya za kufundisha dini.
777652