IQNA

OIC iko tayari kuandaa kikao cha kupambana na ugaidi

11:54 - April 21, 2011
Habari ID: 2109505
Profesa Ikmal Deen Ihsanoghlou, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa jumuiya hiyo iko tayari kuandaa kikao cha kimataifa kwa ajili ya kujadiliwa suala la mapambano dhidi ya ugaidi duniani.
Akizungumza siku ya Jumanne katika kikao cha kupamba na ugaidi huko Strasbourg nchini Ufaransa, Ihsanoghlou amesema kuwa jumuiya ya OIC iko tayari kuandaa kikao kingine kama hicho cha kimataifa kwa ajili ya kujadiliwa tatizo hilo linalozisumbua nchi nyingi duniani. Akibainisha lengo la kufanyika kikao hicho katibu mkuu huyo amesema kwamba kikao hicho ambacho kitawajumuisha wasomi na wanafikra kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu, kitajadili na kuchambua kwa kina tatizo hilo ili kupatikana maana halisi ya neno 'ugaidi' na 'ubaguzi wa rangi'. Amesema baada ya kufanyika kikao hicho, njia na mbinu bora zitawasilishwa kwa ajili ya kupambana kimataifa na tatizo hilo la ugaidi na hivyo kuandaa mazingira bora ya kuwepo amani na utulivu duniani. Amesema kikao hicho pia kitajadili njia za kudhaminiwa gharama na bajeti ya mapambano dhidi ya ugaidi. Kikao cha kupambana na ugaidi cha Strasbourg kilimalizika rasmi hapo siku ya Jumanne. 777656
captcha