IQNA

Mashindano ya kiraa bora ya tartili kuanza leo Imarati

12:43 - April 24, 2011
Habari ID: 2110932
Awamu ya kwanza ya mashindano ya nne ya kiraa bora zaidi ya tartili ya Qur'ani Tukufu yanaanza leo alasiri nchini Imarati kwa hima ya Kamati ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai Ibrahim Muhammad Bumalha amesema kuwa mashindano hayo yanaanza leo alasiri mjini Dubai na kwamba zawadi nono zitatolewa kwa washindi.
Amesema kuwa washindan 493 wa rika zote wanashiriki katika mashindano hayo.
Ahmad Saqar al Suwaidy ambaye ni miongoni mwa wanachama wa kamati hiyo amesema mashindano hayo yanawashirikisha watoto wadogo, vijana na maimamu wa misikiti.
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kiraa bora zaidi ya tartili itafanyika tarehe 15 Mei katika msikiti wa Hassan Sheikh mjini Dubai. 779694


captcha