Wanazuoni na maulama waliohudhuria kikao hicho wamesema kuwa kutokuwepo kwa baraza kama hilo ndilo tatizo na changamoto kuu inayoikabili jamii ya Mashia wa Saudi Arabia na kutaka hati madhubuti ibuniwe kwa lengo la kueneza uhuru wa kifikra, haki za binadamu na uhuru kati ya raia na Waislamu wote wa nchi hiyo.
Juhudi za kulea kizazi bora kinachofahamu vyema utamaduni wa Kiislamu, kuondoa hitilafu miongoni mwa wanazuoni na kuzingatia mielekeo ya kuvumiliana kwenye jamii ni masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho. 779704