IQNA

Wiki ya umoja wa kitaifa yaanza nchini Bahrain

13:37 - April 25, 2011
Habari ID: 2111615
Ratiba maalumu ya kuimarisha umoja wa kitaifa katika fremu ya wiki ya umoja wa kitaifa ilianza kutekelezwa hapo jana Jumapili. Ratiba hiyo inatakelezwa kwa madhumuni ya kupinga dhulma na jinai zinazotekelezwa dhidi ya Wabahrain na ufalme wa nchi hiyo ukishirikiana na ufalme wa Saudi Arabia.
Siku ya kwanza ya kuadhimishwa wiki hiyo imeanza kwa kupigwa nara za kuimarishwa umoja wa wananchi kwa ajili ya kufikiwa malengo na matakwa halali ya kitaifa.
Mipango ya kukabiliana na propaganda za tawala mbili hizo za kifalme za kuzusha mgawanyiko kati ya wananchi wa Bahrain ni mambo mengine yatakayotekelezwa katika kipindi cha wiki hii.
Mungano wa Februari 14 ndio ulioandaa wiki hii ambapo mambo mengine yatakayotekelezwa ni pamoja na kuhudhuria Waislamu kwa wingi misikitini kwa madhumuni ya kusoma Qur'ani Tukufu na dua za kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Wabahrain wote bila kujali madhehebu zao.
Lengo jingine la kuadhimishwa wiki hii ni kulaani kitendo cha kuaibisha na kuchukiza cha falme mbili hizo za kidhalimu cha kubomoa misikiti na kuchoma moto Qur'ani Tukufu. 779932
captcha