IQNA

Wahubiri wa Kiislamu kutoka Liberia watembelea Darul Hadith nchini Iran

17:14 - April 25, 2011
Habari ID: 2111804
Wahubiri watatu wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia kutoka Liberia wametembelea Taasisi ya Darul Hadith mjini Tehran
Akiwakaribisha wageni hao Hujjatul Islam Husseinpur mmoja kati ya wasimamizi wa taasisi hiyo amesema Darul Hadith imeanzishwa kwa lengo la kueneza mafundisho ya Ahlul Bayt AS.
Amesema tovuti ya intaneti ya Darul Hadith (http://www.darolhadith.com) ni kituo cha kutoa majibu ya maswali kuhusu Ahlul Bayt AS kwa waumini kote duniani.
Mhubiri kutoka Liberia, Mahmoud Tipusa ameelezea furaha yake kutembelea kituo hicho na kusema ndio taasisi pekee ya kitaalamu inayoshughulikia Hadithi duniani na kwa hivyo ina nafasi muhimu katika kuhuisha mafundisho ya Ahlul Bayt AS duniani.
Amesema nusu ya watu wote Liberia ni Waislamu na kuongozea kuwa Mashia ni takribani watu elfu mbili. Amesema kuna vyuo kadhaa vya Kishia nchini Liberia na kuongeza kuwa wakaazi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika watapata nuru ya Ahlul Bayt AS.
780680
captcha