IQNA

Kesi ya Mdeni aliyemkosea heshima Mtume Mtukufu (saw) yaanza

17:12 - April 26, 2011
Habari ID: 2112580
Kesi ya Kurt Westergaard, mchora-vikatuni raia wa Denmaki aliyemkosea heshima Mtume Mtukufu (saw) ilianza jana Jumatatu huko Jordan bila ya mhalifu huyo kuwepo mahakamani.
Kwa mujibu wa gazeti la Le Figaro linalochapishwa nchini Ufaransa, Tarek Hawamdeh ambaye ni wakili wa waandishi wa magazeti ya Jordan na mwanasiasa wa nchi hiyo amesema kuwa magazeti na wanaharakati wa kisiasa wa nchi hiyo wameamua kumshtaki Westergaard na vilevile magazeti ya Denmark kwa kukosea heshima Uislamu pamoja na Mtume Mtukufu (saw) katika kesi hiyo inayoendeshwa katika mji mkuu wa Jordan Amman.
Hata hivyo, Nassir Shahada, hakimu anayeendesha kesi hiyo amesema kwamba ameiakhirisha hadi Jumapili tarehe 8 Mei ili apate fursa ya kusikiliza na kuwachunguza mashahidi wa kesi hiyo. Hakimu huyo amesema kuwa ameamua kuendesha kesi hiyo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa magazeti, idhaa na tovuti za intaneti 30 dhidi ya Mdeni huyo. 781075
captcha