IQNA

Ayatullah Qabalan aitisha mkutano wa 'Mshikamano na Bahrain'

17:09 - April 26, 2011
Habari ID: 2112583
Ayatullah Abdul Amir Qabalan, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameitisha mkutano mkuu wa wanazuoni wa Lebanon kwa ajili ya kuonyesha mfungamano na wananchi madhlumu wa Bahrain.
Kwa mujibu wa gazeti la Intiqad la Lebanon, Ayatullah Qabalan ametoa wito huo kufuatia ukandamizaji na jinai kubwa zinazofanywa na askari wa ufalme wa Aal Khalifa na Aal Saud dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Bahrain.
Mkutano huo wa kuonesha mfungamana na taifa la Bahrain umepangwa kuanza saa tano mchana hapo kesho Jumatano katika makao makuu ya baraza lililotajwa la Mashia wa Lebanon.
Jumapili iliyopita pia Ayatullah Qabalan aliwatumia ujumbe Wakristo wa Lebanon akiwatakia pasaka njema na kuelezea matumaini yake kwamba watatumia fursa hiyo ya kidini kuimarisha umoja kati ya Walebanon na hasa Wakristo na Waislamu. 781310
captcha