Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati Sayyid Mohammad Sadeq al Husseini ambaye amezikosoa nchi za Kiislamu kwa kushindwa kuitisha kikao cha dharura cha OIC kujadili mgogoro wa Bahrain.
Amesema maulamaa wengi wa Kisuni pia wameshindwa kutekeleza majukumu yao kuhusu kadhia ya Bahrain.
"Tunatamani tungekuwa Karbala kumsaidia Imam Hussein AS lakini sasa tunawapuuza watu wa Bahrain. Je hao si Waislamu? Je hao si majirani zetu? Tunapaswa kusimama pamoja nao na kutetea haki zao. Watu waliodhulumiwa wa Bahrain wako katika kipindi nyeti cha historia yao. Wana matakwa halali ambayo hata maadui zao wakiwemo Wamarekani na baadhi ya watawala wa Bahrain wanakiri" amesema.
Al Husseini ameongeza kuwa, "leo Bahrain kuna hali ambayo Waziri Mkuu wa Uturuki Rajab Tayib Erdogan ameonya itaibua Karbala nyingine. Wamarekani na vibaraka wao katika eneo hili wana hofu kuwa athari ya harakati ya Wabahraini itaenea katika nchi nyinginezo na hivyo tawala dhalimu katika eneo hili hasa Saudi Arabia zitakuwa na hatima sawa na ya Bahrain".
Aweongeza kuwa "Hii ndio sababu wametuma vikosi vyao Bahrain kukandamiza mwamko wa Kiislamu wa wananchi".
Ametoa wito kwa Waislamu, nchi za Kiislamu, Kiarabu na wote wenye fikra huru duniani kuunga mkono mwamko wa wananchi wa Bahrain.
781110