Kwa mujibu wa Idara ya Wanawake na Masuala ya Familia ya ICRO, kongamano hilo litahudhuriwa na taasisi zisizo za kiserikali kutoka nchi kadhaa. Washiriki wanatazamiwa kutangaza mshikamano wao na harakati ya mwamko wa Kiislamu.
Kati ya nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Algeria, Tunisia, Lebanon, Sudan, Iraq, Syria, Marekani, Japan, Bahrain na Argentina pamoja na mashirika 50 yasiyo ya kiserikali ya wanawake wa Iran na wale kutoka jamii za waliowachache.
Kikao hicho kitamalizika kwa taarifa ya kuunga mkono harakati ya mwamko wa Kiislamu.
782140