Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini Jeff Radebe amesema maoni na mapendekezo kuhusu rasimu ya muswada wa sheria hiyo yatapokelewa hadi Mei 31.
Jumuiya ya Mawakili Waislamu ya Afrika Kusini imepinga sheria hiyo na kuitaja kuwa inayokiuka sheria za Kiislamu kwa sababu inaruhusu mahakama zisizo za Kiislamu kutatua migogoro ya ndoa za Waislamu. Jumuiya ya Wanawake Waislamu ya Afrika Kusini pia imepinga sheria hiyo.
Taasisi kadhaa za Kiislamu nchini Afrika Kusini zimetaka serikali ianzishe mahakama maalumu za Kiislamu ambazo zitashughulikia masuala ya ndoa za Waislamu.
783766