Wakijadili bajeti ya Iran ya mwaka 2011-2012 ambayo inakadiriwa kuwa USD Bilioni 513, wabunge walipitisha muswada wa kuzitaka taasisi zote za kiserikali za kitaifa na kimkoa kutenga asilimia 0.5 ya bajeti kwa ajili ya shughuli za Qur'ani.
Hatua hii imechukuliwa kwa mujibu wa Hati ya Ustawi wa Utamaduni wa Qur'ani nchini Iran. Hati hiyo iliidhinishwa na Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni.
Kwa mujibu wa muswada huo, bajeti ya Shughuli za Qur'ani inapaswa kutumiwa kwa mujibu wa muongozo wa Baraza la Ustawi wa Utamaduni wa Qur'ani.
783903