IQNA

Onyo la al-Azhar kuhusiana na hatari ya kuenea Uwahabi

15:18 - May 02, 2011
Habari ID: 2115840
Ahmad as-Sayeh mhadhiri wa falsafa na itikadi katika Chuo Kikuu cha Kidini cha al-Azhar nchini Misri ameonya dhidi ya hatari ya kuenea fikra potofu za Uwahabi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Akizungumza na televisheni ya al-Alam, As-Sayeh amesisitiza kwamba Uwahabi ni hatari kubwa kwa umma wa Kiislamu. Amesema fikra hizo zinaenezwa duniani kwa ajili ya kuharibu na kuvuruga amani na uthabiti wa ulimwengu wa Kiislamu. Amesema Mawahabi wamekuwa wakieneza fikra ya kubomoa makaburi ya mawalii na viongozi watukufu wa kidini na hivyo kufuata nyayo za mababu zao waliofanya uharibifu mkubwa dhidi ya umma wa Kiislamu.
Ahmad as Sayeh amesema Saudi Arabia ndiyo inayolea na kubuni makundi yenye misimamo mikali ya kupindukia mipaka katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwataka wananchi wa Misri kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kupambana na kundi hilo potofu. Ameongeza kuwa historia ya Misri inathibitisha kwamba Wamisri walikuwa Mashia na kwamba historia hiyo imewafanya kuwa na mapenzi makubwa kwa Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu (saw).
Ahmad as-Sayeh aesisitiza kwamba Chuo Kikuu cha al-Azhar kitaendelea kupambana na Mawahabi na kuandaa mazingira ya kukabiliana na harakati zao za kutiliwa shaka. Amesema hivi karibuni maandamano ya Waislamu yalifanyika nchini Misri dhidi ya Mawahabi na hivyo kudhihirisha chuki ya Wamisri dhidi ya uingiliaji wa Saudi Arabia nchini humo na uungaji mkono wake kwa makundi ya Mawahabi wanaowakufurisha Waislamu. 784508
captcha