IQNA

OIC-IRCICA kupanua zaidi ushirikiano

17:37 - May 02, 2011
Habari ID: 2116029
Mkuu wa masuala ya elimu na utafiti katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Mohammad Reza Dehshiri ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano na Taasisi ya Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu IRCICA.
Akizungumza alipotembelea makao makuu ya IRCICA mjini Istanbul, Dehshiri amepongeza taasisi hiyo kwa juhudi zake za kustawisha utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu.
Naibu Mkuu wa IRCICA Taleb Maruf amekaribisha ujumbe huo na kutoa maelezo kuhusu shughuli za taasisi hiyo.
Mkuu wa masuala ya elimu na utafiti katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Mohammad Reza Dehshiri ambaye ni raia wa Iran ameongoza pia ujumbe wa Iran katika kutembelea IRCICA. Taleb Maruf ametoa wito wa kutiwa saini mkataba wa kuandaa tamasha ya sanaa za Kiislamu katika mji wa Isfahan nchini Iran. Tamasha hiyo itajumuisha nchi 55. Maruf amesema IRCICA pia iko tayari kushiriki katika uchapishaji wa pamoja wa vitabu kuhusu sanaa na historia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
784328

captcha