Akizungumza katika kikao cha Mpango wa Tilawat Noor, Hujjatul Islam Hamid Reza Arbab Suleimani ameongeza kuwa kusoma Qur'ani tu hakutoshi. Amongeza kuwa, 'ni kweli kuwa hata kuangalia aya za Qur'ani kuna thawabu lakini ukweli ni kuwa Qur'ani iliteremshwa kumuongoza mwanadamu kutoka gizani kuelekea katika nuru. Moja ya njia za kuhakikisha mwanadamu anapata muongozo ni kustawisha utamaduni wa kufasiri Qur'ani'.
Ameongeza kuwa hii leo kuna tafsiri kadhaa za Qur'ani ambazo zinaweza kuwaongoza wale wanaotaka kupata mafunzo ya Qur'ani.
784052