IQNA

Mtarjumi wa Qur'ani anapaswa kufahamu vyema Kiarabu

21:53 - May 04, 2011
Habari ID: 2117554
Kuna hatua tatu katika tarjumi ya Qur'ani, muhimu zaidi ikiwa ni mtarjumi kufahamu kikamilifu lugha asili ambayo ni Kiarabu.
Hayo yamesemwa na Salar Manafi Anari, mhadhiri wa lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Allamah Tabatabai mjini Tehran. Amesema kufeli katika hili kunaweza kuibua tarjumi isiyokubalika.
Akizungumza katika kikao cha kuchunguza tarjumi za Qur'ani kwa lugha ya Kiingereza ambacho kimefanyika katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA mjini Tehran mnamo Mei tatu, Dr. Manafi amefafanua kuhusu msingi wa tarjumi kwa mtazamo wa kiakademia. Amesema misingi mitatu ya kutarjumi ni pamoja na kuchunguza kwa kina lugha asili, kufahamu fikra kuu, na kuhamisha fikra hiyo kwa lugha ya pili.
Amesema kuna tafauti kubwa kati ya tarjumi ya Qur'ani na vitabu vinginevyo.
785904
captcha