Hujjatul Islam Walmuslimin Kadhim Seddiqi ameongeza kwamba, mataifa ya eneo yaliyoamka, yana nia ya kufidia makosa yaliyotokea huko nyuma. Sheikh Seddiqi aidha amesema, hivi karibuni pia mataifa ya Ulaya yaliyodhalilishwa kwa miaka mingi na madola ya kibeberu nayo pia yataaamka, na harakati ya kutaka uadilifu itaenea duniani kote.
Sambamba na kuonyesha masikitiko yake kuhusiana na kuuawa wananchi wasio na hatia wa Libya na Yemen, Khatibu wa sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, madola makubwa yanayodai kutetea demokrasia na uhuru hivi sasa yanafikiria kuchukua rushwa kutoka kwa madikteta waliopitwa na wakati kama vile Muammar Gaddafi wa Libya na Ali Abdullah Saleh wa Yemen. Pia ameelezea wasiwasi wake juu ya kuendelea kuuawa Waislamu wasio na hatia wa Bahrain na kuongeza kwamba, mioyo ya Waislamu imeingiwa na huzuni kubwa kutokana na vitendo vya kinyama vinavyofanywa na utawala uliooza wa Aal Khalifa huko Bahrain.
787433