Msafara huo utaondoka mjini Durban Afrika Kusini mapema mwezi Juni kwa njia ya nchi kavu na kupitia Botswana, Zambia, Kenya, Ethiopia, Sudan, Misri na hatimaye Ghaza. Msafara huo wa misaada ya Ghaza utapita njia ya kilomita 10000 katika kusini, mashariki na kaskazini mwa Afrika. Msafara huo pia unalenga kuwafahamisha Waafrika kuhusu kadhia ya Palestina na mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Msafara huo umesheheni misaada mbalimbali vikiwemo vifaa vya ujenzi, madawa, misaada ya kibinadamu na majenereta ya umeme.
Tayari Waislamu nchini Sudan wamesema wataukaribisha msafara huo wakati utakapowasili nchini humo.
Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Afrika Kusini (South African Relief Agency) lina makao yake mjini Durban na linalenga kutoa misaada kwa wanaohitajia kitaifa na kimataifa.
788173