IQNA

IQNA kuandaa kikao cha "Vyombo vya Habari na Qur'ani"

17:17 - May 09, 2011
Habari ID: 2119290
Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA limeandaa kikao chenye anwani ya "Vyombo vya Habari na Qur'ani" ambacho kitafanyika katika makao ya IQNA mjini Tehran Jumanne Mei 10.
Kikao hicho kimeandaliwa kwa ushirikiano na Kamati ya Misikiti na Sanaa nchini Iran. Kikao hicho ni katika mfululizo wa mijadala kuhusu nafasi na utendaji kazi wa misikiti na taasisi za kiutamaduni katika kustawisha utamaduni wa Qur'ani nchini Iran.
Sayyid Abbas Anjam mkuu wa masuala ya tilawa katika Kanali ya Televisheni ya Qur'an ya Iran na Saeed Sa'adat Mkuu wa Masuala ya Misikiti katika mkoa wa Ardebil ni kati ya watakaohutubia kikao hicho.
Kikao hicho pia kitachunguza mpango wa 1444 ambao ulifanyika kwa muda wa siku sitini mwaka jana kote nchini Iran ukijumuisha mashindano na kozi kuhusu Suratul Kahf. Mpango huo ulitekelezwa na Kanali ya Televisheni ya Qur'ani kwa ushirikiano na taasisi kadhaa za Qur'ani za Iran. Watu 81 lefu walishiriki katika mashindano hayo kwa njia ya simu ambapo elfu 10 walifanikiwa kuihifadhi kikamilifu Suratul Kahf.
788471
captcha